KANUNI YA 50/30/20: NJIA RAHISI YA KUIWEKA KATIKA MAISHA HALISI TANZANIA

UTANGULIZI 

Leo nakuletea silaha moja rahisi inayoitwa Kanuni ya 50/30/20. Haijalishi unalipwa Tsh 300,000 au Tsh 3,000,000. Kanuni hii itakusaidia kujua kila shilingi yako inaenda wapi.

Watu wengi huko Marekani na Ulaya wameitumia of miaka mingi. Leo tunaiweka kwenye hali halisi ya Tanzania, bila stress.

Mwanamke akipanga bajeti ya mshahara wake kwa kutumia kanuni ya 50/30/20

Kanuni ya 50/30/20 Ni Nini?

Ni njia rahisi ya kugawa mshahara wako katika vikundi 3 tu.

Mtaalamu wa fedha Elizabeth Warren ndiye aliyebuni kanuni hii. Wazo lake ni moja: panga pesa yako kabla pesa ikupange wewe.

Kanuni inasema hivi:

1. 50% ya mshahara wako iende kwenye mahitaji Muhimu

2. 30% iende kwenye matamanio 

3. 20% iende kwenye Akiba na Kulipa madeni.

Sehemu ya 1: 50% - Mahitaji muhimu bila haya huwezi kuishi.

Hii ni nusu ya mshahara wako. Tsh 500,000 kama unalipwa Tsh 1,000,000, haya ni mambo ambayo kama hutayalipa, maisha yako yanasimama.

- Kodi ya Nyumba

- Chakula cha mwezi - Mchele, maharage, mafuta

- Umeme, Maji, Gesi

- Usafiri wa kwenda Kazi - dala dala, bajaji 

- Bima ya afya na matibabu 

- Bando la Kazi - kama kazi yako inategemea mtandao

Tahadhari hapa: Simu mpya sio hitaji,  Netflix sio hitaji, hizi ni 30%. Kama 50% yako imezidi  kuna shida, huenda unakaa nyumba ghali sana au unakula nje kila siku. Hapo ndio pa kuanza kukata.

Sehemu ya 2: 30% - matamanio nataka, sio lazima 

Hii ndio sehemu inayowafanya watu wengi kukosa pesa. 30% ya mshahara wako. Tsh 300,000 kama unalipwa Tsh 1,000,000.

Ni nini kinaingia hapa?

Haya ni mambo yanayokufurahisha lakini maisha yataendelea bila yake.

- Kutoka na Marafiki - Mgahawa, Club

- Soda, Juice, Nje ya Chakula cha Nyumbani

- Netflix, DSTV, Data ya TikTok

- Nguo mpya, viatu

- Safari za burudani

- Zawadi 

Kanuni inakupa ruhusa ya kutumia hapa. Tatizo ni watu wengi wanatumia 70% hapa,tumia 30% yako kwa amani, ukimaliza, ngoja mwezi ujao.

Sehemu ya 3: 20% - Akiba na mustakabali lipa wewe wa Kesho

Hii ndio sehemu inayokutofautisha na masikini. 20% ya mshahara wako, Tsh 200,000 kama unalipwa Tsh 1,000,000.

Unatakiwa kufanya nini nayo?

1. Akiba ya dharura: anza kuweka hadi ufike miezi 3-6 ya matumizi yako, hii ni kwa ajili ya magonjwa, kufukuzwa kazi.

2. Kulipa Deni: Kama una mkopo, lipa zaidi ya kiasi cha chini.

3. Kuwekeza: ukiishaweka akiba, anza kuweka kwenye biashara ndogo, hisa, au ardhi. 

Kanuni hapa ni moja: Toa hii 20% kwanza. Pesa ikiingia, peleka kwenye akaunti nyingine kabla hata hujagusa 50% na 30%.


Mfano halisi: hebu tumia kwa mtu wa Dar es Salaam, tuseme Amina anapokea Tsh 800,000 kwa mwezi.

50% - Mahitaji: Tsh 400,000

- Kodi: Tsh 150,000

- Chakula: Tsh 150,000 

- Usafiri + Umeme + Maji: Tsh 100,000 = Tsh 400,000 

30% - Matamanio: Tsh 240,000

- Kula nje na marafiki: Tsh 80,000

- Bando + Netflix: Tsh 40,000

- Nguo na vipodozi: Tsh 120,000 = Tsh 240,000 

20% - Akiba: Tsh 160,000

- Weka kwenye CRDB au NMB akaunti ya akiba = Tsh 160,000 

Hakuna fujo, Kila kitu kina mahali pake.

Makosa 3 watu huyafanya wakijaribu Kanuni hii

1. Kuchanganya 30% na 50%

Kunanunua iPhone 15 kwa sababu nayo ni hitaji la kazi, hapana, Simu ya Tsh 150,000 inafanya kazi ile ile, tofauti ni 30%.

2. Kusahau 20%

Wengi wanasema nitaweka akiba nikibakiza, hivyo huwezi kubakiza, toa kwanza.

3. Kujilinganisha 

Rafiki yako anatumia 50% kwenye matamanio. Wewe endelea na mpango wako, baada ya miaka 2 utaona matokeo.

Jinsi ya Kuanza leo - hatua 3 tu

Usisubiri mwezi ujao.

1. Kaa dakika 10: Chukua mshahara wako wa mwezi uliopita,  uligawa vipi? Uko karibu na 50/30/20?

2. Fungua Akaunti 2: akaunti 1 ya Matumizi, Akaunti 1 ya Akiba.

3. Mshahara ukiingia: Peleka 20% kwenye akiba, kisha gawa 50% na 30% kwenye akaunti ya matumizi.

HITIMISHO 

Uhuru wa Kifedha Unaanza na hesabu rahisi, kanuni ya 50/30/20 sio uchawi, ni nidhamu. Inakupa ruhusa ya kutumia pesa bila hatia. Inakulinda kwa dharura, na inajenga mustakabali wako. Usijaribu kuwa perfect. Kama mwezi huu umetumia 55/25/20, sawa mwezi ujao jaribu 52/28/20, muhimu ni kuanza.

Sasa na wewe: Kama unalipwa Tsh 600,000, 20% yako ni kiasi gani? Andika jibu kwenye comment 👇

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUJENGA AKIBA YA DHARURA HATA KAMA KIPATO NI KIDOGO

JINSI YA KUIANZA SAFARI YAKO YA UHURU WA KIFEDHA