TABIA ZA KILA SIKU ZINAZOHARIBU MPANGO WAKO WA FEDHA BILA KUJUA
Je unafahamu mpango wako wa kifedha unaharibiwa na vitu gani? Mara nyingi, si maamuzi makubwa tu yanayouvuruga mpango wa kifedha, bali tabia ndogo za kila siku zinazoonekana ndogo lakini zikiungana zinakula kipato chako kwa kiasi kikubwa. Makala hii inaonesha tabia baadhi na jinsi ya kuanza kuzibadilisha au kuziacha. Tabia ya 1: Kutoandika matumizi yako ya kila siku Kitendo cha kutokujua pesa zinaishia wapi mara nyingi kunatokana na kutokuandika matumizi yako ya kila siku. Mfano; matumizi ya chakula, usafiri, vocha, na mambo mengine. Usipoandika utatumia pesa bila mpangilio maalumu na utashangaa pesa zinaisha kabla ya siku ulizopanga au matumizi yanakuwa nje ya mpango uliojiwekea. Hivyo kutoandika matumizi yako ni tabia inayoharibu mpango wako wa kifedha taratibu bila kujua na hatimaye utakusababishia kutokuwa na uhuru wa kifedha Suluhisho : Ili uweze kurekodi matumizi yako tumia daftari dogo au app rahisi kama app ya notes kuandika kila matumizi yako ya kila siku hata kama ...