KARIBU KWENYE PESA HATUA KWA HATUA
Karibu kwenye Pesa hatua kwa hatua mahali pa kujifunza kuhusu fedha kwa lugha rahisi ya Kiswahili.
Lengo la kuanzisha blog hii ni kuhakikisha tunakusaidia katika masuala ya fedha ikiwemo kupanga bajeti, kuepuka madeni na jinsi ya kuanzisha biashara ndogo ndogo.
Kwenye Pesa Hatua kwa Hatua utapata makala zinazokusaidia:
- Kupanga bajeti yako hata kama kipato ni kidogo
- Kuanzisha na kukuza biashara ndogo ndogo
- Kuondoka kwenye madeni kwa mpango unaoeleweka
- Kujenga tabia ya kuweka akiba na kuwekeza kidogo kidogo
Makala zote zitakuwa kwa Kiswahili, zikielezea kila jambo kwa urahisi, bila maneno magumu ya kifedha. Lengo letu ni kukusaidia uanze safari ya uhuru wa kifedha kutoka pale ulipo sasa bila presha, bila aibu, hatua kwa hatua.
Kama ni mara yako ya kwanza kutembelea blog hii, nakuomba ujiunge na safari:
Soma makala za bajeti na madeni kama hatua ya kwanza
Hifadhi blog hii (bookmark) kwenye simu yako ili urudi kirahisi
Niandikie maoni au ujumbe kama una swali lolote au mada unayotaka tuijadili
Asante kwa kutembelea Pesa Hatua kwa Hatua. Tuanzie hapa na twende pamoja, hatua moja baada ya nyingine, mpaka pesa ziwe rafiki yako na siyo adui wako.
Maoni
Chapisha Maoni